마태복음 22장 Swahili NT
- 1 Yesu alisema nao tena kwa kutumia mifano:
- 2 "Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi.
- 3 Basi, akawatuma watumishi kuwaita walioalikwa waje arusini, lakini walioalikwa hawakutaka kufika.
- 4 Akawatuma tena watumishi wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa: karamu yangu iko tayari sasa; fahali wangu na ng'ombe wanono wamekwisha chinjwa; kila kitu ni tayari, njoni arusini.
- 5 Lakini wao hawakujali, wakaenda zao; mmoja shambani kwake, mwingine kwenye shughuli zake,
- 6 na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatukana, wakawaua.
- 7 Yule mfalme akakasirika, akawatuma askari wake wakawaangamize wauaji hao na kuuteketeza mji wao.
- 8 Kisha akawaambia watumishi wake: Karamu ya arusi iko tayari kweli, lakini walioalikwa hawakustahili.
- 9 Basi, nendeni kwenye barabara na wowote wale mtakaowakuta waiteni waje arusini.
- 10 Wale watumishi wakatoka, wakaenda njiani, wakawaleta watu wote, wabaya na wema. Nyumba ya arusi ikajaa wageni.
- 11 "Mfalme alipoingia kuwaona wageni, akamwona mtu mmoja ambaye hakuvaa mavazi ya arusi.
- 12 Mfalme akamwuliza, Rafiki, umeingiaje hapa bila vazi la arusi? Lakini yeye akakaa kimya.
- 13 Hapo mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno."
- 14 Yesu akamaliza kwa kusema, "Wengi wamealikwa, lakini wachache wameteuliwa."
- 15 Kisha, Mafarisayo wakaenda zao, wakashauriana jinsi ya kumnasa Yesu kwa maneno yake.
- 16 Basi, wakawatuma wafuasi wao pamoja na wafuasi wa kikundi cha Herode. Wakamwuliza, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu, na kwamba wafundisha njia ya Mungu kwa uaminifu; humwogopi mtu yeyote, maana cheo cha mtu si kitu kwako.
- 17 Haya, twambie maoni yako. Je, ni halali au la, kulipa Kaisari?"
- 18 Lakini Yesu alitambua uovu wao, akawaambia, "Enyi
- 19 Nionyesheni fedha ya kulipia kodi." Nao wakamtolea sarafu ya fedha. sarafu ya fedha.
- 20 Basi, Yesu akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?"
- 21 Wakamjibu, "Ni vya Kaisari." Hapo Yesu akawaambia, "Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu."
- 22 Waliposikia hivyo wakashangaa; wakamwacha, wakaenda zao.
- 23 Siku hiyo, baadhi ya Masadukayo walimwendea Yesu. Hao ndio wale wasemao kwamba wafu hawafufuki.
- 24 Basi, wakamwambia, "Mwalimu, Mose alisema mtu aliyeoa akifa bila kuacha watoto, lazima ndugu yake amwoe huyo mama mjane, amzalie ndugu yake watoto.
- 25 Sasa, hapa petu palikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa kisha akafa bila kujaliwa watoto, akamwachia ndugu yake huyo mke wake mjane.
- 26 Ikawa vivyo hivyo kwa ndugu wa pili, na wa tatu, mpaka wa saba.
- 27 Baada ya ndugu hao wote kufa, akafa pia yule mama.
- 28 Je, siku wafu watakapofufuka mama huyo atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba? Maana Wote saba walimwoa."
- 29 Yesu akawajibu, "Kweli mmekosea kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu wala nguvu ya Mungu!
- 30 Maana wafu watakapofufuliwa hawataoa wala kuolewa, watakuwa kama malaika mbinguni.
- 31 Lakini kuhusu suala la wafu kufufuka, hamjasoma yale aliyowaambieni Mungu?
- 32 Aliwaambia, Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Isaka na Yakobo! Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai."
- 33 Ule umati wa watu uliposikia hivyo ukayastaajabia mafundisho yake.
- 34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja.
- 35 Mmoja wao, mwanasheria, akamwuliza Yesu kwa kumjaribu,
- 36 "Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu katika Sheria ya Mose?"
- 37 Yesu akamjibu, "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili yako yote.
- 38 Hii ndiyo amri kuu ya kwanza.
- 39 Ya pili inafanana na hiyo: Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.
- 40 Sheria yote ya Mose na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili."
- 41 Mafarisayo walipokusanyika pamoja, Yesu aliwauliza,
- 42 "Ninyi mwaonaje juu ya Kristo? Je, ni mwana wa nani?" Wakamjibu, "Wa Daudi."
- 43 Yesu akawaambia, "Basi, inawezekanaje kwamba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu Daudi anamwita yeye Bwana? Maana alisema:
- 44 Bwana alimwambia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.
- 45 Basi, ikiwa Daudi anamwita Kristo Bwana, anawezaje kuwa mwanawe?"
- 46 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumjibu neno. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kumwuliza swali.